Welcome/Karibu sana!

Karibu sana/Welcome!

We provide an inspirational forum for people with challenges in life,businesses,education etc to exchanges ideas and share the solutions to the globe.We are mainly focused on youths who are especially facing many challenges in life.Mobile no:+255653259644

Looking for something?

Subscribe to this blog!

Receive the latest posts by email. Just enter your email below if you want to subscribe!

Wednesday, 21 October 2015

Daktari feki aambukizaUkimwi watu 100

Mwanaume mmoja aliyejidai kuwa daktari na kuwaambukiza watu zaidi ya mia moja virusi amefikishwa mahakamani nchini Cambodia.
Yamkini daktari huyo bandia alikuwa akiwadunga wagonjwa wake kwa sindano aliyokuwa ameitumia kwa mgonjwa aliyekuwa na virusi vya Ukimwi.
Yem Chhrin anakabiliwa na kosa la kuua na kuambukiza watu ugonjwa huo kwa kukusudia.
Aidha Bw Yem anashtakiwa kwa kuwalaghai watu kuwa ni daktari ilhali hana vyeti halali vya kuhudumia umma.
Iwapo atapatikana na hatia mahakama ya nchi hiyo huenda ikamhukumu kifungo cha maisha jela.
Waathiriwa walioambukizwa maradhi ya Ukimwi wanatokea katika kijiji cha Roka kilichoko Kaskazini Magharibi.
Mmoja wao ni kiongozi wa kidini wa madhehebu ya Buddha na mtoto wa miaka mitatu.
Takriban 10 kati ya waathiriwa hao wanakisiwa kuwa wameshakata roho.
Kwa mujibu wa ripoti za mahakama daktari huyo bandia amekiri kuhudumu bila vyeti maalum ila anakana kukusudia kuwaambukiza watu hao 100 virusi vinavyosababisha maradhi ya Ukimwi

No comments :

Post a Comment