NEC yavionya vyama vya siasa kuacha kutoa taarifa za uongo kwa wafuasi wao.
Tume
ya taifa ya uchaguzi (NEC) imevionya vyama vya siasa kuacha kutoa
taarifa za uongo kwa wafuasi wao dhidi ya tume hiyo na badala yake watoe
taarifa sahihi kuhusu tume na kujikita kuwaelimisha wafuasi wao na
wananchi kujitokeza kupiga kura Oktoba 25 mwaka huu.
Onyo hilo limetolewa na kamishna wa tume hiyo Bi. Mary Longway
wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa na watendaji wa tume
hiyo mjini Songea mkoani Ruvuma.
Kamishna huyo amesema kama vyama vya siasa vitawahamasisha wafuasi
wao kubaki kwenye vituo vya kupigia kura kutakuwa na uwezekano wa
kutokea vurugu zitakazowatisha wapiga kura kujitokeza kupiga kura huku
kaimu mwenyekiti wa Chadema mkoani Ruvuma Bw. Rashid Chitepete akisema
ni lazima wawe jirani na vituo vya kupigia kura ili kuwepo na watu wa
kuwatangazia matokeo.Naye kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma ACP Mihayo Msikhela
amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuhubiri amani kwa wafuasi wao
No comments :
Post a Comment