![]() |
- Watu wengi wanawaza kuwa yamkini EL angefaa kuwa mgombea urais kupitia CCM mwaka 2015. Kwa upande wangu naona na ninaamini hivi, Edward Lowassa hafai kabisa kuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM kwa sababu:-
- Tuhuma dhidi yake kuwa ni fisadi mkubwa kwenye sakata la Richmond na hatimaye Dowans. Tuhuma hizi haziwezi kusafishika kwa namna yoyote. Labda tu ataje kwamba hahusiki na akiri hadharani (press conference) kwamba yuko tayari kutoa ushahidi mbele ya umma na mahakama wa kuwezesha kuwatia hatiani wahusika ambao wamemvisha kengere shingoni mwake.
- Uvumi kwamba yeye amejitajirisha kwa njia zisizohalali; kwani, utajiri wake hauelezeki ulivyopatikana. Hapa kunatuhuma kwamba akiwa waziri wa Aridhi aliuza na kutoa viwanja vingi vya umma kwa matajiri wa kihindi na wafanyabiashara kadhaa. mf, uwanja wa wazi wa karibu na majengo ya Bora (Kijitonyama-Mabatini). Aidha, tuhuma za kuyatoa maeneo ya kiwanja cha UVCCM akishirikiana na E. Nchimbi pale Dar es Salaam.
- Tuhuma za kujenga makundi ndani ya CCM, mathalan, wakati wa uchaguzi uliopita kumpitisha J. Kikwete. Alimpaka matope Salim A. Salim, Philip Mangula, Fredrick Sumaye na wengine wengi.
- Katika uchaguzi wa ndani ya chama Edward Lowassa ametuhumiwa kutumia fedha nyingi mno kuhonga wajumbe wa chama kwa ngaszi mbali mbali ili apitishe watu wanaomuunga mkono yeye ndani ya chama, mathalan, wakuu wa wilaya na mikoa; wenyeviti na makatibu wa ccm ngazi ya wilaya na mikoa.
- Tuhuma za ushiriki wake katika biashara ya madawa ya kulevya akishirikiana na familia ya mkuu wa kaya.
- Ni mpenda vyeo na king'ang'anizi.
- Mtoa rushwa kwa kuhonga taasisi za dini ili asafishike na kujijenga na kutengeneza mazingira ya kupigiwa debe na viongozi wa dini.
- Ni tu mwenye kupendelea watu wa jamii yake au watu wanaotokea upande wa kwao kaskazini. Kwa ufupi ni mkabila.
No comments :
Post a Comment