Muda mfupi uliopita, mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF,
Maalim Seif Sharif Hamad, ameitisha mkutano wa waandishi wa habari na
kusema kuwa baada ya chama chake kukusanya fomu zote za matokeo kutoka
vituoni, yeye amepata kura 200,007 dhidi ya kura 178,363 za mgombea wa
CCM anayetetea nafasi yake, Dk. Ali Mohammed Shein, na kuitaka Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo halisi kama yalivyo kwenye
fomu zinazotoka vituoni.
No comments :
Post a Comment