Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki Moon akiwa na Rais Barack Obama kwenye ikulu ya White House.
Wito wa Bw Obama wa kupunguza kiwango cha utoaji hewa chafu cha
asilimia 32 chini ya viwango vya 2005 kufikia 2030 umepingwa na viwanda
vikubwa vya Marekani vikisema ni kinyume cha sheria na kuwa gharama yake
ni kubwa.
Baada ya kukutana na Bwana Obama katika ikulu ya White House,
kiongozi huyo wa umoja wa mataifa amesema kuhusiana na mabadiliko ya
hali ya hewa anaunga mkono pendekezo la rais Obama tangu siku ya kwanza
alipoingia ofisini.
Bw Obama amesema tishio la mazingira kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ni swala nyeti linaloikabili dunia.
Kiongozi huyo wa marekani amesema mkutano wa kujadili mazingira utakaofanyika Paris mwezi desemba lazima ufanikiwe.
No comments :
Post a Comment