Maisha ya mamilioni
ya watu barani Afrika yamo hatarini iwapo aina mpya ya vimelea vya
Malaria vinavyopatikana barani Asia vitaenea na kufika barani Afrika.
Watafiti wameonya kuwa vimelea hivyo havisikii dawa aina ya Artemisinin inayotumika kote barani Afrika kutibu Malaria.
Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la watabibu
la 'Journal Nature Communications' unaonesha kuwa aina ya mbu
anayepatikana Afrika, Anopheles ambaye hulaumiwa kwa kueneza vimelea vya
malaria hana kinga yeyote dhidi ya vimelea hivyo hatari.
Watafiti
hao kutoka Marekani wameonya kuwa endapo hilo litatokea kwa sababu moja
au zaidi basi maisha ya watu wengi haswa watoto yatakuwa hatarini.
Daktari Rick Fairhurst, kutoka kituo cha utafiti wa
maradhi yanayoambukiza 'National Institute of Allergy and Infectious
Disease (NIAID)',nchini Marekani aliyeongoza utafiti huo anasema kuwa
anatumai kuwa utafiti huu labda utatoa changamoto kwa utafiti zaidi
kufanyika kutafuta mbinu mpya ya kukabiliana na ugonjwa wa Malaria
unaoenea mashariki mwa Asia.
Anasema kuwa aina hiyo mpya ya
Malaria ilipatikana mara ya kwanza nchini Cambodia mwaka wa 2008, lakini
sasa imeenea hadi Mashariki mwa Asia na kuleta maafa makubwa zaidi.
Shirika la afya duniani WHO imeonya kuwa iwapo aina
hiyo mpya ya malaria itaenea na kuishinda nguvu dawa nambari moja kwa
matibabu ya Malaria yaani artemesenin basi maendeleo yaliyopatikana
katika kipindi cha miaka 15 iliyopita itatokomea.
WHO ilitoa
utafiti ulioonesha kuwa idadi ya vifo vinavyotokana na Malaria imepungua
kwa kiasi cha asilimia 60% kote duniani katika kipindi cha miaka 15
iliyopita
No comments :
Post a Comment