KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape
Nnauye amepata ajali mbaya akiwa njiani kuelekea Lindi akitokea jijini
Dar es Salaam.
Nape amenusurika kifo katika ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi katika
eneo la Njia Nne Kilwa akiwa anatoka Dar kuelekea jimboni kwake.
Nape ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama, Lindi alipata ajali
hiyo baada ya tairi la mbele la gari aliyokuwa akiendesha aina ya
Toyota Land Cruiser kupasuka na kupinduka mara kadhaa katika eneo la
Nyangao mkoani Lindi.
Katika gari hilo, Nape alikuwa peke yake na ndiye alikuwa akiendesha
gari hilo ambapo amepata majeraha madogo ila anaendelea vizuri.
Akizungumza na mtandao huu wa BITZ, Nape amesema: "Namshukuru Mungu nimetoka
salama na nawaomba wananchi wasiwe na hofu japo ajali ilikuwa mbaya
maana gari lilipinduka mara kadhaa, nimepata majeraha madogomadogo na
michubuko ila ni mzima.
Gari limeharibika vibaya ila ninachoshukuru nilikuwa nimefunga mkanda na 'air bag' nazo zimenisaidia."
Kabla ya ajali hiyo, Nape alikuwa jijini Dar es Salaam ambapo aliungana
na mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli aliyekuwa na
mikutano kadhaa ya kampeni katika jiji la Dar na baada ya shughuli hiyo
alikuwa akirejea Lindi kuendelea na kampeni kwenye jimbo lake la Mtama.
No comments :
Post a Comment