Waziri mkuu wa
Israel Benjamin Netanyahu amekosolewa baada ya kudai kuwa kiongozi wa
kidini mpalestina alimshawishi aliyekuwa kiongozi wa kimila wa Ujerumani
Adolf Hitler kutekeleza maauaji ya kimbari ya wayahudi.
Kiongozi
mkuu wa kidini mjini Jerusalem Haj Amin al Husseini kwa muda mrefu
amekuwa akituhumiwa kuwa anaunga mkono mauaji ya kimbari ya wayahudi.
Lakini katika hotuba yake kwenye mkutano wa kimataifa wa wayahudi, bwana Netanyahu ameendeleza shutuma hizo.
Kulingana
naye, Hitler alitafuta maoni kutoka kwa kiongozi huyo wa kidini
kuhusiana na ari yake ya kuwafurusha wayahudi barani Ulaya.
Kwa maelezo yake Netanyahu, kiongozi huyo alimwambia Hitler kuwa wayahudi wote wangeenda Palestina iwapo angewafukuza Ulaya.
Na Hitler alipomuuliza,afanye nini ?
Netanyahu, anasema kuwa kiongozi huyo alimshauri Hitler "awateketeze wayahudi"
Wataalam wa maswala ya historia hata hivyo wamekuwa wakipuuzilia mbali madai hayo kuwa siyo ya kweli.
Viongozi wa upinzani nchini Israel wametaja madai ya Netanyahu kama historia ya kupotosha.
Viongozi
wa kipalestina kwa upande wao wamesema matamshi hayo yanaonyesha jinsi
Waziri huyo mkuu wa Israeli anawachukia wapalestina.
No comments :
Post a Comment