Matokeo ya awali ya kura zilizopigwa siku ya jumamosi huko Nigeria zinaonesha kuwa kiongozi wa upinzani Muhammadu Buhari
anaongoza kwa zaidi ya kura milioni mbili zaidi ya mpinzani wake wa karibu ambaye ni rais Goodluck Jonathan.Generali
Buhari wa chama cha All Progressives Congress (APC) anaonekana
kusajili matokeo mema mapema hata kabla ya kuhesabiwa kwa kura za mjini
Lagos.Matokeo ya uchaguzi mkuu nchini
Nigeria yanatarajiwa kutangazwa saa chache zinazokuja wakati majimbo
yaliyosalia yakisubiriwa kutangaza matokeo yao.Huku zaidi ya nusu
ya matokeo yakiwa yametangazwa mgombea wa upinzani Muhammadu Buhari
yuko mbele ya rais wa sasa Goodluck Jonathan.Hata hivyo matokeo bado hayawezi kutabiriwa kwa kuwa majimbo yenye watu wengi kama Lagos na Rivers hayajatangaza matokeo yake.Mwandishi wa BBC mjini Abuja amesema mchuano bado ni mkali.
No comments :
Post a Comment