Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria,INEC, Attahiru Jegaamemtangaza
rasmi Kiongozi wa wa chama cha upinzani cha Nigeria jenerali Muhammadu
Buhari kuwa rais wa taifa hilo kubwa barani Afrika baada ya kumbwaga
rais wa zamani Goodluck Jonathan.Tayari
rais anayeondoka
madarakani Goodluck Jonathan amekwisha kubali kushindwa kwake baada ya
kumpigia simu mpinzani wake, Jenerali Buhari na kumpongeza kwa ushindi
huo wa kihistoria.Hii inakuwa mara ya kwanza katika historia ya taifa
hilo kwa rais wa nchi hiyo kung'olewa madarakani na kiongozi wa
upinzani.
Wadadisi wa maswala ya ndani wanasema kuwa inaonekana kuwa Nigeria sasa imekomaa kisiasa haswa baada ya kushuhudia mapinduzi kadha ya kijeshi tangu ipate uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1960.
Hata hivyo kumekuwa na taharuki kubwa haswa baada ya tume ya uchaguzi kuchelewa kutoa matokeo ya uchaguzi.
No comments :
Post a Comment