Mshindi wa uchaguzi wa urais nchini
Nigeria Muhammadu Buhari anasema kuwa ushindi wake unamaanisha kuwa
taifa hilo linafuata mfumo wa kidemokrasi.Buhari alimshinda
mpinzani wake Goodluck Jonathan,kwa kura millioni 2 idadi ambayo
wachanganuzi wanasema kuwa itazuia harakati zozote za kuanzisha kesi.Ni mara ya kwanza kwa rais wa taifa hilo kushindwa katika uchaguzi.
Bwana Buhari ,kiongozi wa zamani wa kijeshi alichukua mamlaka mnamo mwaka 1980 kupitia mapinduzi.Hatahivyo
alifanya kampeni za kidemokrasia kwa lengo la kutaka kusafisha siasa
katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika.Katika
hatua ya kidemokrasia,rais anayeondoka Goodluck Jonathan alimpigia simu
Buhari kukubali ushindi na vilevile kutoa taarifa akiwataka wafuasi wake
kukubali matokeo
No comments :
Post a Comment