Wapiganaji waliofunika nyuso zao wameshambulia eneo la chuo kikuu cha
Garissa kaskazini mwa Kenya karibu na mpaka wa taifa hilo na
Somalia.Milio mikali ya risasi pamoja na milipuko imesikika katika chuo
kikuu cha Garissa mjini humo.Maafisa wa usalama wa Kenya wamethibitisha kuwa watu wawili wamefariki huku wanne wakijeruhiwa.Wakaazi wa eneo hilo wametakiwa kukaa mbali na eneo la chuo hicho.Haijulikani
ni nani aliyekusika na shambulizi hilo ,lakini kundi la wapiganaji wa
Somalia Al shabaab limetekeleza misururu ya mashambulizi mjini Garissa
pamoja na maeneo mengine ya Kenya tangu mwaka 2011 wakati wanajeshi wa
kenya walipopelekwa Somalia
No comments :
Post a Comment