Siku moja baada ya Wakala wa Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na
Majini (SUMATRA) kutangaza kupungua kwa mwendo kasi wa mabasi yaendayo
mikoani hadi kufikia spidi 80, wasafiri jijini Mwanza wamekumbana na adha
kubwa ya kukosa usafiri baada ya mabasi kutoka Dar es Salaam kushindwa
kufika kwa wakati mjini hapa.
Katika stendi kuu ya mabasi eneo la Nyegezi jijini hapa, wasafiri hao
walisema kauli hiyo ya serikali itawaumiza, hivyo wameiomba kuwasaidia
kwa kuisihi iruhusu safari kwa mwendokasi wa kawaida, vinginevyo wao
ndiyo wanaopata maumivu.Endelea hapa...
No comments :
Post a Comment