Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh. Jaji Mstaasfu Damiani Lubuva.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa zoezi la upigaji kura ya
maoni ya Katiba Inayopendekezwa, halitafanyika kama ilivyokuwa
imepangwa hapo awali kufanyika Aprili 30 mwaka huu hadi hapo
itakapotangazwa tena.
NEC imetoa sababu kuwa, kuahirishwa kwa zoezi hilo ni kutokana na
kutokamilika kwa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura
ambapo mpaka sasa ni mkoa mmoja tu wa Njombe ndio umeanza na
haujakamilisha zoezi hilo ambalo linatakiwa lifanyike kwa mikoa yote 30
ya Tanzaia.
NEC imeongeza kuwa, zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mkoa wa Njombe litakamilika April 18 na baada ya hapo zoezi
litafuatia mikoa ya Ruvuma, Iringa, Mtwara na Lindi.
Vifaa vya kuandikishia (BVR kits) vingine 248 vitawasili ndani ya wiki ijayo na vingine 1600 vitafuata baada ya muda mfupi.
No comments :
Post a Comment