Arsenal walifufua
matumaini yao katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa ushindi wa kusisimua
dhidi ya Bayern Munich katika uwanja wa Emirates mechi iliyochezwa
Jumanne usiku.
Matumaini ya Gunners yalikuwa yamefifia baada yao
kushindwa mechi zao za kwanza katika ligi hiyo msimu huu ugenini Dinamo
Zagreb na nyumbani dhidi ya Olympiakos.
Lakini vijana hao wa
Arsene Wenger walionyesha bado hawako tayari kusalimu amri kwa kulaza
Bayern, ambao wamekuwa wakiogopwa sana siku za karibuni.
Bayern
walidhibiti mpira zaidi lakini Arsenal walifunga kupitia nuguvu mpya
Olivier Giroud dakika ya 77 baada ya kipa Manuel Neuer kufanya kosa
nadra sana na kushindwa kufikia frikiki iliyopigwa na Santi Cazorla.
Walijihakikishia ushindi sekunde za lala salama Mesut Ozil alipofunga kutokana na krosi ya Hector Bellerin.
Arsenal wanafaa kumshukuru sana kipa wao Petr Cech,
aliyerejea kulinda michuma baada ya makosa ya David Ospina mechi yao
dhdi ya Olympiakos, aliyeokoa mipira hatari kutoka kwa Thiago Alcantara
na Arturo Vidal.
Neuer pia alikuwa amefanya miujiza yake kabla ya
kosa hilo, akiokoa mpira wa kichwa wa Theo Walcott kwa ustadi mkubwa
kipindi cha kwanza.
Katika mechi nyingine, Chelsea walitoka sare tasa na Dynamo Kiev.
Haya ndiyo matokeo ya mechi zote za Ligi ya Klabu Bingwa zilizochezwa Jumanne:
BATE Bor 0 - 2 Barcelona
Bayer Levkn 4 - 4 Roma
Arsenal 2 - 0 Bayern Munich
Dynamo Kiev 0 - 0 Chelsea
Dinamo Zagreb 0 - 1 Olympiakos
FC Porto 2 - 0 Maccabi Tel Aviv
Valencia 2 - 1 KAA Gent
Zenit St P 3 - 1 Lyon
No comments :
Post a Comment