Chelsea walitoka
sare tasa mechi yao ya tatu katika Kundi G kwenye mechi ya Ligi ya Klabu
Bingwa Ulaya ugenini dhidi ya Dynamo Kiev.
Vijana hao wa Jose Mourinho waligonga mlingoti wa goli mara mbili na pia wakanyimwa penalti.
Eden Hazard alikaribia sana kufunga, lakini kipa Oleksandr Shovkovskiy akagongesha mpira wake kwenye mlingoti.
Winga
wa Dynamo Kiev Andriy Yarmolenko alishambulia sana kutoka kulia lakini
aliishia kupokonywa mpira. Alipokonywa mpira mara 25 kwenye mechi hiyo.
Chelsea
walifaa kupewa penalti baada ya Cesc Fabregas kuanguka alipokabiliwa
vikali na Serhiy Rybalka lakini refa hakusikia kilio chao.
Frikiki
ya Willian iligonga mwamba wa goli kabla ya Asmir Begovic kumzuia
mchezaji mwenyeji Derlis Gonzalez kuwafunga Chelsea kwenye mechi hiyo
iliyochezewa Ukraine.
Vijana hao wa Mourinho sasa wameshinda mechi moja pekee kati ya tano walizocheza majuzi zaidi katika mashindano yote.
Hata
hivyo, uchezaji wao ulionekana kuimarika pakubwa Ulaya tangu
walipolazwa na Porto Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2-1 ugenini Septemba 29.
Ushindi
wa Porto 2-0 dhidi ya Maccabi Tel-Aviv unawafanya Chelsea kusalia
nambari tatu kundini wakiwa na alama nne, moja nyuma ya Kiev na alama
tatu nyuma ya viongozi wa kundi Porto
No comments :
Post a Comment