
Kampuni ya Tigo imetoa gawio la shilingi bilioni 3.8 kwa
wateja wa TIGO PESA katika robo ya tatu ya mwaka huu ambalo ni sawa na
ongezeko la asilimia 17 la gawio la shilingi bilioni 3.3 lililotolewa
robo ya pili.
Meneja mawasiliano wa TIGO, JOHN WANYANCHA amesema gawio hilo
linawahusu wateja binafsi, mawakala wa rejareja na washirika wengine wa
TIGO PESA na mteja atapata gawio kulingana na wastani wa salio la kila
siku lililotunzwa kwenye akaunti yake ya TIGO PESA
No comments :
Post a Comment