
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akifungua pazia kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa
jengoa makazi na biashara la Cictoria Place linalojengwa na NHC katika
eneo la Victoria jijini Dar es salam Octoba 20,2015. Kushoto ni Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela kairuki na
kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu
Waziri mkuu MIZENGO PINDA ameyataka mashirika na kampuni za
ujenzi nchini kujenga nyumba za makazi zenye ghorofa ndefu ili
watanzania wengi wapate fursa ya kupata nyumba.
Akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za ghorofa pacha za
Victoria place unaofanywa na shirika la nyumba – NHC- jijini DSM, PINDA
amesema ujenzi shadidi unahusisha nyumba za gorofa ndefu ambao hutumia
eneo dogo na hivyo hupunguza matumizi makubwa ya ardhi.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa NHC, NEHEMIA MCHECHU amesema ujenzi wa nyumba
hizo utagharimu shilingi bilioni 30.3 na utahusisha nyumba za makazi
88, eneo la kuegeshea magari na maduka makubwa.
No comments :
Post a Comment