
Katibu mkuu wa UMOJA wa MATAIFA BAN KI MOON amefanya ziara
ya kushtukiza katika mji wa JERUSALEM nchini ISRAEL ikiwa ni juhudi za
umoja wa mataifa kutaka kumaliza ghasia zinazoendelea nchini humo kati
ya wapalestina na waisrael.
BAN ametoa wito kwa pande zote mbili kujiondoa katika hatari ya
mivutano ya kidini na kuwa na majadiliano yenye kuleta maana kwa pande
zote mbili.
Pia ameonya kuwa hatua za dharura zinastahili kuchukuliwa ili kuzuia machafuko hayo kusambaa zaidi.Waziri mkuu wa ISRAEL BENJAMIN NETANYAHU ameilaumu PALESTINA kwa
kuanzisha vurugu na kukanusha tuhuma za nchi yake kutumia nguvu
kudhibiti makabiliano hayo na kusisitiza kuwa taifa lake linajilinda.BAN pia anatarajia kukutana na rais wa PALESTINA MAHMOUD ABBAS katika UKINGO WA MAGHARIBI.
No comments :
Post a Comment