Rais
Kikwete amemkabidhi IGP Mangu funguo za magari hayo katika Chuo Kikuu
cha Mafunzo ya Polisi Kurasini jijini Dar es salaam katika sherehe ya
kukabidhi magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia
utendaji kazi wa jeshi la polisi
Rais JAKAYA KIKWETE ameliagiza Jeshi la Polisi nchini
kuendelea kufanya kazi kwa weledi kama ilivyokuwa wakati huu wa kampeni
za uchaguzi ili kuhakikisha Taifa linamaliza uchaguzi Mkuu kwa amani na
utulivu.
Rais KIKWETE ametoa agizo hilo Jijini DSM wakati wa akikabidhi magari
399 ya jeshi la polisi ikiwa ni utekelezaji wa programu ya maboresho
kwa Jeshi la Polisi nchini.
Kwa mujibu wa Rais KIKWETE, katika kipindi hiki ambapo kampeni za
uchaguzi mkuu ujao zinaelekea kumalizika, Jeshi la polisi nchini
limefanya kazi nzuri katika kulinda raia na mali zao.
Magari hayo 399 yaliyokabidhiwa na Rais KIKWETE ni miongoni mwa
Magari 777 yaliyoombwa na Jeshi la Polisi nchini kwa ajili ya kufanya
kazi ya kulinda raia pamoja na mali zao.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi MATHIAS CHIKAWE
ametoa wito kwa Watendaji wa Jeshi la Polisi nchini kuyatumia magari
hayo kwa malengo yaliyokusudiwa.
No comments :
Post a Comment