Tume ya Taifa ya Uchaguzi - NEC imewahakikishia Wananchi na
Viongozi wa Vyama vya siasa nchini kuwa imeboresha Mfumo wa kuhesabu
kura kwa katika uchaguzi mkuu ujao, tofauti ya mfumo uliotumika katika
uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Kauli hiyo hiyo ya NEC imetolewa mkoani MBEYA na Afisa Habari Mkuu wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi,- GIVENESS ASWILE wakati wa mkutano wa tume
hiyo na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa mkoani humo.
Mkutano huo wa Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Viongozi wa
Vyama vya siasa mkoani MBEYA ni mwendelezo wa mikutano inayofanywa na
NEC na Wadau mbalimbali wa uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi huo
unafanyika katika mazingira ya amani na utulivu
No comments :
Post a Comment