Rais Dr. JAKAYA KIKWETE amesema kuwa TANZANIA inaimarisha
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania -JWTZ, siyo kwa nia ya
kumchokoza mtu au nchi yoyote, bali kwa nia ya kulinda mipaka yake kwa
sababu kila hatua ya maendeleo ina changamoto tofauti za ulinzi wa nchi.
Aidha, Rais KIKWETE amebainisha kwamba siyo uharibifu kutumia fedha nyingi kujenga Jeshi, kama ambavyo baadhi ya watu wanavyodai, kwa sababu ni wajibu wa kila nchi kuhakikisha kuwa Jeshi lake linakuwa katika utayari wa kukabiliana na uchokozi wa aina yoyote.
Rais amesema uchumi wa TANZANIA, na hasa uchumi mpya wa gesiasilia, ambayo utakuwa msingi mkuu wa uchumi na maendeleo ya TANZANIA lazima ulindwe kwa njia yoyote na kwa nguvu zote.
Dr. KIKWETE aliyasema hayo katika sherehe ya kukamilisha mradi wa ukarabati wa uwanja wa ndege wa kurushia ndegevita na sherehe ya kufungua mradi wa kuongeza urefu wa uwanja wa ndegevita katika kituo cha kijeshi cha kamandi ya anga cha NGERENGERE, mkoa wa MOROGORO.
Rais KIKWETE ambaye pia ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya TANZANIA ameishukuru nchi ya Jamhuri ya Watu wa CHINA kwa kuisaidia TANZANIA katika masuala ya ulinzi.
CHINA ndio inagharimia miradi hiyo miwili ya maboresho ya Uwanja wa ndegevita wa NGERENGERE ambao ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuhudumia hata ndege kubwa za abiria ikitokea hali ya dharura.
Ikulu

No comments :
Post a Comment