Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid ya Hispania Christiano Ronaldo ameingia tena katika headlines baada ya kutwaa tuzo nyingine ya ufungaji bora. Christiano Ronaldo ambaye September 30 aliweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Real Madrid kwa kufunga jumla ya goli 324 na kuvunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Raul Gonzalez.
October 13 Christiano Ronaldo alipokea kiatu cha dhahabu baada ya kuibuka mfungaji bora wa Ulaya
kwa kufunga magoli mengi katika mechi zinazohushisha mechi za ndani ya
nchi husika kwa kufunga jumla ya goli 48 katika mechi 35. Ronaldo amechukua kiatu cha dhahabu cha tatu akiwa na Real Madrid baada ya mara ya kwanza kutwaa tuzo hiyo akiwa Man United msimu wa 2007/2008.
Kwa ujumla Ronaldo
anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo hiyo mara nne,
huenda ukawa unajiuliaza namna au mfumo unaotumika kutoa tuzo hiyo, tuzo
hii uhusisha wachezaji wanaotokea katika Ligi zote barani Ulaya tofauti ni Ligi Kuu Uingereza,Hispania,Italia na Ujerumani zinakuwa na pointi 2 kwa kila goli huku ligi zingine zikiwa na point1.5 hadi 1 baada ya hapo point inazidishwa na idadi ya magoli aliyofunga mchezaji ndio mshindi anapatikana.
No comments :
Post a Comment