Watanzania kwenye
mitandao ya kijamii wamekuwa wakitumia kitambulisha mada #DearNyerere kumkumbuka
mwanzilishi wa taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Sikukuu ya Nyerere
Dei huadhimishwa kila Oktoba 14 kukumbuka siku aliyofariki kiongozi huyu.Watanzania
wamekuwa wakitumia vitambulisha mada kadha kueleza hisia zao kuhusu maono
aliyokuwa nayo Mwl Nyerere wakati wa uhuru 1961 na hali ilivyo sasa. Mwandishi
wetu pia amezungumza na baadhi ya wakazi ambao wanasema mengi ya maono ya
Mwalimu Nyerere hayajatimia.Vitambulisha mada vingine vinavyotumiwa ni
#NyerereDay #NyerereDaySpecial na #NyerereQuotes ambapo Watanzania wanakumbuka
nukuu muhimu za kiongozi huyo.Mwalimu Nyerere alizaliwa Aprili 13, 1922 na
akafariki Oktoba 14, 1999.Aliongoza Tanzania hadi alipostaafu 1985.Aliendelea
kuwa mwenyekiti wa CCM hadi 1990. Alifariki kutokana na saratani aina ya
leukemia akitibiwa London.
No comments :
Post a Comment