Hivi karibuni kumezuka kundi la matangazo ya jobrize.com ambapo unatakiwa kujiunga kwenye mtandao huo then unapewa namba ambayo kadiri uitangazavyo kwa watu na kuunganisha watu wengi zaidi akaunti yako inaingiza pesa.Jambo hili si mara ya kwanza kutokea mwaka 2013 kulitokea jambo kama hili ila wao walijiita bepaid.com.Nilifanikiwa kujiunga binafsi na mtandao huo nilifight sana kuweza kutangaza namba niliyopewa ila mwishowe baada ya kufikisha kama kiasi cha dola 3000 nilitaka kudai pesa ile ila cha kushangaza nikaambiwa nijaze survey form,nikaijaza na hapo ndio ilikua mwisho wa ile habari.Watanzania tusidanganyike na huu mtandao ni uongo mtupu,wala tusipoteze muda katika kujiunga na huu mtandao.
No comments :
Post a Comment