Vikosi maalum vya majeshi na jeshi la Polisi vinaonekana katika
mitaa mbali mbali ya kisiwa cha Unguja pamoja na hali kuonekana ni
shwari na salama.
Lengo lao kuu ikiwa ni kuimarisha ulinzi lakini wakazi mbali mbali wa
kisiwa hicho wana maoni tofauti Salum Mwalim ni naibu katibu mkuu
Chadema Zanzibar na mgombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Kikwajuni
anasema hadhani hili ni suala la kulinda amani tu “angalia Tanganyika
ina wakazi zaidi ya millioni 44 lakini huoni vikosi maalum huoni
wanajeshi wakiranda randa mitaani..lakini ukija Zanzibar leo kila kona
unakutana na askari...jambo ambalo linawajengea hofu wananchi.”
Vikosi vya usalama Zanzibar
Kwa baadhi ya wakazi wa upande wa Unguja wao walikuwa na maoni
tofauti Hajji Suleiman mkazi wa Kilimani anasema inategemea na mazingira
ya eneo na kwa eneo wanakoishi watu anaona ni mazuri na si mabaya ila
kwa wengine askari wanaotembea mitaani si wazuri sana wanapiga watu bila
kisa wakiwa wamekaa maskani.
Bolcher Juma anasema hawa ni kama watu wa kawaida wanaolinda ila hawajulikani wanalinda vipi maana wako kila mahali.
Ali Othmani Maulid anasema hii ni moja ya usalama wao kwasababu hata
yeye atakuwa hana spidi ya kufanya tukio lolote kama kuna askari
anayewalinda
No comments :
Post a Comment