Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi
-CCM Balozi ALI ABEID KARUME amesema wazanzibari wana mamlaka kamili ya
kuchagua kiongozi mzuri wanaomtaka kuiongoza ZANZIBAR.
Balozi KARUME ameyasema hayo katika kongamano la kujadili mwenendo wa
kampeni ya uchaguzi mkuu 2015 lililoandaliwa na taasisi ya NYUMBA YA
HAMASA.
Amesema mamlaka ya ZANZIBAR ilirudishwa kwa wazanzibari baada ya
kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi ambapo awali yalikuwa mikononi mwa
Baraza la Kwanza la Mapinduzi.
Naye kada wa Chama Cha Mapinduzi Balozi AMINA SALUM ALI amesema ni
vema kwa vyama vya siasa kuweka wazi ilani za vyama vyao ili kuhakikisha
wananchi wana uelewa wa kutosha kuhusu ilani hizo jambo ambalo
litawasaidia kuchagua viongozi wanaofaa kuongoza nchi.
Wadau wa kongamano hilo wamesema uundwaji wa serikali ya umoja wa
kitaifa kumesaidia kwa Zanzibar kurejesha hali ya umoja , amani na
utulivu
No comments :
Post a Comment