Mamlaka
ya udhibiti wa maji na nishati -EWURA imezionya kampuni za mafuta
kuacha kufanya hujuma yoyote ile ya kulikosesha taifa nishati hiyo
wakati wa uchaguzi mkuu kwa kuwa kuna hazina ya kutosha ya nishati hiyo
nchini huku wamiliki wa kampuni hizo wakiomba ulinzi wa ziada kipindi
hiki.
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Felix Ngalamgosi amesema iwapo
mafuta yatakosekana katika kituo chochote kile nchini watakichukulia
kuwa ni hujuma na wahusika watachukuliwa hatua stahili ikiwemo
kunyang'anywa leseni na kuwa kuanzia sasa wameimarisha ukaguzi katika
vituo vya mafuta.
Kwa upande wao wakuu wa makampuni hayo wamesema wanahofia usalama
wa maghala yao na vituo vya mafuta kwani katika uchaguzi jambo lolote
ikiwemo vurugu vinaweza kutokea hivyo wameiomba serikali kuimarisha
ulinzi katika maeneo hayo.
Mkurugenzi mkuu wa EWURA amewaambia wakuu hao wa makampuni ya
mafuta kuwa watanzania hawana kawaida ya kufanya vitendo vya uvunjifu wa
amani wala uharibifu wakati wa uchaguzi lakini hata hivyo serikali
itaimarisha ulinzi katika maeneo yanayohifadhi mafuta.
No comments :
Post a Comment