Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi katika Mahakama kama ifuatavyo;
Rais amemteua Bi. Katarina Revocati kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania (Chief Registrar). Kabla ya uteuzi huu, Bi. Revocati alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani.Rais pia amemteua Ndugu John Rugalema Kahyoza kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani na kabla ya uteuzi huu, Ndugu Kahyoza alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu.Mwingine aliyeteuliwa ni Ndugu Ilvin Claud Mugeta ambaye anakuwa Msajili wa Mahakama Kuu. Kabla ya Uteuzi huu ndugu Mugeta alikua Mkurugenzi wa Ukaguzi na Maadili.Uteuzi huu umeanza tarehe 3 Oktoba,2015.MWISHO
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
19 Oktoba, 2015
No comments :
Post a Comment