Wakati
muda wa uchaguzi ukielekea ukingoni baadhi ya wazee na watu wasiojua
kusoma na kuandika hasa wa maeneo ya vijijini wamebainika kushindwa
kutofautisha picha za wagombea urais, ubunge na udiwani zilizoko
kwenye karatasi za kura jambo linaloweza kuwasababishia washindwe
kuwachangua viongozi wanaowatarajia.
Tatizo hilo limebainishwa na baadhi ya wagombea udiwani wa vyama
vinavyounda (UKAWA) ambao wamesema pamoja na kutumia muda mwingi
kuwaelimisha tatizo hilo ni kubwa na elimu zaidi inahitajika na
wameendelea kuwaomba watanzania kuona umuhimu wa kufanya mabadiliko kwa
kumchagua Mh.Lowassa kwani ndiye mwenye uwezo wa kumaliza matatizo
hayo.
Wananchi wanakabiliwa na tatizo la kutokujua kusoma na kuandika
wamesema limekuwa likiwasababishia kushindwa kutekeleza majukumu yao
ipasavyo,kukosa,haki zao za msingi na kushindwa kutunza siri zao.
Wakiwa katika maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima mwanzoni
mwa wiki viongozi wa idara ya elimu mkoa wa Arusha wamesema
wanaendelea kupunguza idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika
kupitia mpango wa kupeleka huduma ya elimu katika maeneo waliko na
wanapofanyia shughuli zao.
Arusha ni miongoni mwa mikoa yenye idadi kubwa ya watu wasiojua
kusoma na kuandika ambapo kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 kati
ya watu 1,694,310 wanaojua kusoma na kuandika ni 1,372,391 na
wasiojua kusoma ni 321,918 takwimu ambazo hata hivyo zitakuwa
zimebadilika katika kipindi hiki cha kufuikia mwaka 2015.
No comments :
Post a Comment