Zikiwa
zimesalia siku tano tu ili taifa liingie kwenye zoezi la uchaguzi
mkuu,baadhi ya viongozi wa dini na wanasiasa mkoani Rukwa, wametoa wito
kwa tume ya taifa ya uchaguzi ifanye kikao cha maridhiano na vyama vya
siasa,ili kuwe na kauli moja juu ya siku ya upigaji kura kuliko ilivyo
hivi sasa,ambapo wakati tume inasema watu wakipiga kura warudi majumbani
wanasiasa wanahamasisha watu wakae umbali uliowekwa kisheria kulinda
kura zao.
Viongozi hao wakiongea kwenye jukwaa la amani lililoandaliwa na
asasi ya Sumango mjini Sumbawanga,wamesema kauli hizo mbili
zinazokinzana kwa kiasi kikubwa,zinaleta mkanganyiko mkubwa kwa wananchi
ambao wanazisikia kutoka pande hizo mbili,na kama isipofanyika juhudi
ya makusudi zinaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani,kwa kuzua ghasia
siku ya kupiga kura na kuathiri zoezi zima la uchaguzi mkuu.
Akiongea kwenye jukwaa hilo la amani kabla na baada ya uchaguzi
mkuu, mratibu wa muungano wa asasi za kiraia wilayani Sumbawanga Sumango
Bw.Vicent Kuligi,amesema lengo la kufanyika kwa jukwaa hilo ni
kuwakutanisha viongozi wa ngazi mbalimbali mkoani Rukwa,ili wajadili
namna bora ya kuienzi na kuitunza amani iliyopo, kwani zoezi la uchaguzi
mkuu mara kwa mara limekuwa likiacha majeraha mbalimbali katika taifa
No comments :
Post a Comment