Mwili
wa kijana Odva Makenge aliyezama maji baada ya gari walilokuwa
wamepanda ndani ya kivuko cha kigamboni kutumbukia baharini umeonekana
kando ya bahari ya Hindi eneo la Ocean Road huku famili ya marehemu
ikilalamikia polisi kikosi cha wanamaji kwa kushindwa kuchukuwa hatua
haraka.
Wakizungumza na ITV wakiwa katika hospitali ya taifa Muhimbili
ambako mwili wa marehemu umepelekwa kwa uchunguzi ndugu zake wamesema
walikuwa wameamua kufanya jitihada binafsi kutafuta wazamiaji na kuitaka
serikali kuwachukulia hatua wafanyakazi wa kivuko kwa kushindwa
kusimamia sheria za ndani ya pantoni pamoja na kukaa kimya baada ya
tukio.
Akijibu malalamiko hayo kamanda wa kikosi cha wanamaji Mboje Kanga
amesema mtoa taarifa alipeleka taarifa polisi wa kikosi cha usalama
barabarani badala ya kikosi cha wanamaji hivyo kuchelewa kwa taarifa
kumechangia wao kuchelewa kuchukuwa hatua na kueleza jitihada
walizofanya katika kuutafuta mwili huo.
Gari lililohusika na tukio hilo lina namba za usajili T252 CFW aina
ya Toyota Marck two ambalo bado halijaonekana na dereva anashikiliwa na
polisi kikosi cha wanamaji kwa mahojiano na chanzo cha ajali hiyo
inadaiwa ni ulevi.
No comments :
Post a Comment