Kutambuliwa
kwa mahujaji hao kunafanya idadi ya mahujaji wa Tanzania waliopoteza
maisha katika ajali hiyo kufikia ishirini na tano (25).
Majina
kamili ya mahujaji hao ni Bi. Faiza Ahmed Omar na Bi. Rehema Ausi
Rubaga kutoka kikundi cha Khidmati Islamiya pamoja na Bw. Masoud Juma
Khamis kutoka Kikundi cha Ahlu Dawaa.
Hadi
sasa mahujaji kumi na tano (15) kutoka Tanzania bado hawajulikani
walipo na jitihada za kuwatafuta bado zinaendelea. Aidha, miili ya
mahujaji kumi na tisa (19) kutoka Tanzania tayari imeshazikwa nchini
Saudi Arabia.
Serikali
ya Saudi Arabia inaendelea kutoa taarifa zaidi za kuwatambua mahujaji
waliofariki dunia au kujeruhiwa katika ajali hiyo na Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu
wahanga wa ajali hiyo kadri itakapokuwa inazipokea.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
19 Oktoba, 2015
No comments :
Post a Comment