Tume
ya taifa ya uchaguzi NEC imeviomba vyama vya siasa kutumia majukwaa ya
siasa katika kipindi hiki kifupi kuelezea sera za vyama vyao ili
kuwasaidia wananchi kufanya maamuzi sahihi na kuepuka lugha za uchochezi
zinazoweza kuhatarisha maisha ya watanzania.
Kamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi Profesa Amon Maligha
amelazimika kutoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa tume na
viongozi wa vyama vya siasa mkoani Mtwara.
Amesema tume imeanza kushuhudia uvunjifu wa maadili ya uchaguzi
katika kipindi hiki cha kampeni ikiwa ni pamoja na lugha za uchochezi na
kejeli zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani na hivyo kutumia fursa hiyo
kuwaasa viongozi wa vyama vya siasa kuepuka kushawishi ama kuhamasisha
mambo yanayoweza kuvuruga amani.
Kwa upande wake msimamizi wa tume ya uchaguzi kanda ya kusini
Grecensia Mayala amesema vifaa vya uchaguzi vimekuwa vikiingia katika
mkoa wa Lindi na Mtwara kwa awamu na hivi sasa mikoa hiyo imeanza
kupokea karatasi za kupigia kura na kusafirishwa katika majimbo
No comments :
Post a Comment