Mwanasheria
mkuu wa serikali Bwana George Masaju amewataka watanzania kuzingatia
katiba, sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza uchaguzi mkuu kwa kuwa
zimwekea msingi na haki na wajibu wa kila mtanzania, vyama vya siasa,
wagombea na wadau ili kufanikisha uchaguzi kwa amani na utulivu.
Akizungumza katika kongamano la kuombea amani katika uchaguzi mkuu,
Bwana Masaju amesema sheria ya taifa ya uchaguzi katika kifungu cha 104
inakataza kufanyika mikusanyiko umbali wa mita 200 kutoka kituo cha
kupigia kura masharti ambayo yanamtaka kupiga kura wanapaswa kurejea
katika makazi yao ili kupisha wengine kupiga kura.
Kwa upande wake mwakilishi wa sheikh mkuu wa mkoa Shekh Maulid
Mwakidede amewataka wananchi kutambua hakuna taaluma yeyeto kama hakuna
amani katika nchni nchi yeyote, huku mkuu wa Patriki Mission Bwana Nbele
Mwaselela akiwataka wanasiasa, wananchi na wanaharaki kuhacha kutumia
lugha ya kashfa na matusi katika mikutano yao na wananchi na kutambua
kunamisha baada ya uchaguzi mkuu
No comments :
Post a Comment