Mgombea
wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na vyama
vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Edward Lowassa ameahidi
kuboresha mpaka wa Tunduma kwa kuufanya kuwa wa kisasa zaidi huku
akiahidi kuufanya ufanye kazi kwa saa ishirini nne tofauti na ilivyo
hivi sasa.
Kwa mara ya pili mji wa kibiashara wa Tunduma wamdhihilishia Edward Lowassa.
Siku sita pekee zikiwa zimesalia ujumbe ni mmoja tu kwa watanzania.
Freeman Mbowe mwenyekiti wa Chadema amewataka watanzania kujitokeza
wingi kupiga kura huku akiwahakikisha hakuna kura hata moja
itakayoibiwa.
Katika siku ya mwisho ya mikutano ya kampeni kanda ya nyanda za juu
kusini, Kingunge Ngombale Mwiru anasema nchi iko tayari kwa sasa kwa
mabadiliko.
Baada ya kuhutubia mikutano saba iliyokuwa imesheheninidadikubwa
zaidi ya wananchi Edwrad Lowassa akatumia jukwaa la mkutano mjini
Tunduma kutatua kero kubwa ya msongamano.
Mgombea huyo pia amewahakikishia watanzania kuwa kama watamchagua
atahakikisha anaongoza kwa misingi ya katiba na sheria huku akiwaahidi
uchumi imara.
No comments :
Post a Comment