Mgombea
urais wa CCM Dr John Pombe Magufuli ameendelea kuwa kivutio kwa wapiga
kura huku akiwataka wakazi wa kanda ya ziwa wanaoendesha shughuli za
uvuvi katika ziwa Victoria wametakiwa kuluitunza ziwa hilo na kutotumia
sumu aina ya Thiodani kuvua samaki kwa lengo la kutoua mazalia ya samaki
ili wananchi waweze kuendesha shughuli za uvuvi kwa muda mrefu na
kujiingizia kipato binafsi na serikali kwa ujumla.
Mgombea urais wa chama cha mapinduzi Dr John Pombe Magufuli
ameendelea kuwa kivutio na alama ya kiongozi mzalendo kwa kupata
mapokezi makubwa kutoka kwa wananchi wanaojipanga barabarani wakati
akielekea katika mikutano yake licha ya uwepo wa mvua ili kumuona lakini
pia kumsikia huku wakiamini kuwa Dr Magufuli ndie rais wao wa awamu ya
tano kwa mujibu wa nyimbo wanazoimba.
Akiwa katika jimbo la Buchosa mkoani Geita licha ya kwamba ni
mapema asubuhi huku mvua ikinyesha wananchi hao wameonekana kutojali
mvua kwa kumpa mapokezi ya kuvunja rekodi katika jimbo hilo ambapo
akizungumza nao Dr John Pombe Magufuli amewataka wakazi wa kanda ya ziwa
kutovua samaki katika ziwa Victoria kwa kutumia sumu ili waweze
kuendesha shughuli za kiuchumi zinazotegemea ziwa hilo kwa muda mrefu
kwa faida ya nchi na vizazi vijavyo.
Akiwa njiani kutoka katika jimbo la Buchosa kuelekea jimbo la Nkome
lililoko Geita vijijini Dr Magufuli amezuri eneo la chimbuko lake
katika kijiji cha katoma kwa kutembelea makaburi ya babu zak mkoa wa
Geita ni miongoni mwa mikoa inayolima zao la nanasi kwa kiasi kikubwa na
hapa Dr Magufuli anawaahidi wananchi hao kujenga kiwanda cha kuongeza
thamani ya zao hilo ili wananchi waweze kunufaika kiuchumi tifauti na
sasa ambapo mananasi hayo yanauzwa kwa bei ya chini jambo ambalo
halimnufaishi mkulima
No comments :
Post a Comment