Dr Magufuli amewataka watanzania kuendelea kudumisha muungano na amani ya nchi.
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imewahakikishia watanzania wote na jumuia za
kimataifa kuwa uchaguzi mkuu utafanyika kwa uhuru, haki na kwa amani
huku akionya wale wote hasa vijana wanaojaribu kuhatarisha amani ili
kuuvuruga uchaguzi huo huku mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dr John Pombe Magufuli akiwataka watanzania kuendelea kudumisha
muungano na amani ya nchi.
Kabla ya kuelekea Pemba visiwani Zanzibara mgombea urais wa chama
cha mapinduzi Dr John Pombe Magufuli amefanya mikutano ya hadhara katika
maeneo ya Kisarawe mkoani Pwani na kisha jimbo la Ukongo jijini Dar es
Salaam.
Mara baada ya mikutano hiyo Dr John Pombe Magufuli akiwa ndie
waziri mwenye dhamana na ujenzi akashuhudia utiaji sahihi wa makubaliano
ya ujenzi wa mradi wa barabara ya juu yaani fly over katika eneo la
Tazara jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kipaumbele cha serikali ya
awamu ya nne ilikuwa kuiunganisha mikoa yote kwa barabara za lami na
sasa kipaumbele ni kupunguza msongamono wa magari katika majiji ya
Tanzania.
Mara baada ya shughuli hiyo Dr John Pombe Magufuli akaelekea Pemba
visiwani Zanzibar na kufa nya mkutano wa hadhara Pemba ambapo
amewatahadharisha watanzania kuwa makini na wale aliowaita mamluki
wanaounea wivu muungano wa Tanzania na Zanzibar.
Nae mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha mapinduzi Dr
Mohamed Shein akawahakikishia watanzania na jumuia za kimataifa uchaguzi
huru,haki na wa amani na kuwaonya wale wote wanaotaka kuleta chokochoko
No comments :
Post a Comment