Kiongozi wa chama
kikuu cha upinzani nchini Guinea amejiondoa katika uchaguzi uliofanyika
nchini humo akisema kuwa kulikuwa na udanganyifu mkubwa uliotekelezwa na
serikali kulingana na kiongozi wake wa kampeni.
Uamuzi huo wa
Cellou Diallo wa kujiondoa unajiri wakati ambapo matokeo yanaonyesha
kwamba rais Alpha Conde anaongoza kwa wingi wa kura akitafuta kushinda
awamu ya pili ya miaka mitano.
Wachunguzi kutoka muungano wa Ulaya wanasema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa haki licha ya matatizo makubwa ya vifaa.
Matokeo kamili ya uchaguzi huo yanatarajiwa mwishoni mwa wiki hii.
No comments :
Post a Comment