Mgombea mwenza wa chama cha demokrasia na maendeleo
–CHADEMA, JUMA DUNI HAJI amewaomba wakazi wa mjini KIGOMA kukichagua
chama hicho ili kiweze kujenga miundo mbinu ya Reli, barabara, huduma
za maji, afya na kuboresha sekta za umeme, kilimo na uvuvi.
Akiwaomba wananchi kukichagua chama hicho DUNI amesema wamejipnga vema kuboresha huduma za jamii zikiwemo huduma za elimu.
JUMA DUNI HAJI ametoa ahadi hizo wakati wa kampeni zilizofanyika mjini KIGOMA.
Mapema makada mbalimbali kutoka baadhi ya vyama vya upinzani walinadi
madiwani, mgombea mwenza na mgombea urais kupitia umoja huo na kusema
wamejipanga kwa ajili ya kuwatumikia wananchi ili waweze kupata
maendeleo ya kiuchumi na kijamii
No comments :
Post a Comment