Msongamano mkubwa
wa magari umeshuhudiwa katika moja ya barabara kuu za kuingia jiji la
Nairobi baada ya lori kuanguka na kufuziba upande mmoja wa barabara.
Wengi
wa wakazi waliokuwa wakijiandaa kwenda kazini kutumia barabara hiyo ya
Uhuru Highway karibu wamelazimika kutumia muda mwingi kufika jijini.
Ajali hiyo ilitokea usiku mita chache baada ya kupita mzunguko wa barabara wa Museum Hill ukielekea Nairobi.
Magari yanayotaka kuingia jijini yanaelekezwa kutumia barabara ya Kijabe Street, mwandishi wa BBC Bashkas Jugsoday anasema.
Eneo hilo liko karibu na chuo kikuu cha Nairobi.
Hakuna ripoti zozote za majeruhi.
Barabara
hiyo hutumiwa na watu wanaotoka maeneo ya magharibi mwa jiji na pia
magharibi mwa nchi kama vile Naivasha na Nakuru, Eldoret na Kisumu
No comments :
Post a Comment