Rais JAKAYA KIKWETE amefungua majengo ya Hazina, Benki Kuu
Tawi la DODOMA na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za
Serikali mjini DODOMA.
Akizungumza baada ya Ufunguzi wa Majengo hayo, Rais KIKWETE amesema
serikali inaendelea kuuandaa mji wa DODOMA ili uweze kupokea Makao Makuu
ya Serikali ukiwa na Miundombinu yote muhimu,
Amesema ukuaji wa uchumi unaoonekana hivi sasa ni matokeo ya utendaji kazi mzuri wa Benki Kuu.Kwa upande wake Waziri wa Fedha SAADA MKUYA SALUM amesema kukamilika
kwa majengo hayo ni utekelezaji wa maagizo ya serikali ya kujenga na
kuendeleza makao makuu ya serikali mjini DODOMA.Amesema kuanzishwa kwa Kanda ya Kati ya Benki Kuu ni ushahidi wa kukua kwa shughuli za Kiuchumi
No comments :
Post a Comment