Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi -CCM ABDULRAHMAN KINANA
ameendelea na kampeni za kumnadi mgombea urais kupitia chama hicho Dkt.
JOHN MAGUFULI katika mikoa ya KATAVI na RUKWA ambapo pamoja na mambo
mengine amesema serikali ya awamu ya tano itakayoundwa na CCM
itarekebisha sheria kufanya biashara na nchi jirani.
Akizungumza katika mikutano ya kampeni KINANA amesema sheria hizo ni
za muda mrefu na hivyo zinapaswa kufanyiwa marekebisho ili kutoa haki ya
msingi kwa wakazi wanaoishi mikoa ya mipakani kutembeleana na ndugu
zao pamoja na kutoa fursa ya kutumia mipaka kuimarisha biashara zao.
Amesema mara baada ya kuundwa serikali ya awamu ya tano chini ya
CCM atamshauri Rais wa serikali hiyo Dkt. JOHN MAGUFULI kufuta sheria
hiyo na kuruhusu wananchi hao badala ya kutumia hati ya kusafiria
watumie vitambulisho vya kupigia kura kuvuka kwenda nchi jirani.
Akiwa mkoni KATAVI, KINANA amewaasa wakazi wa mkoa huo kutopiga kura
kwa ushabiki na badala yake wamchague Dkt. MAGUFULI ili asimamie
maendelo hasa katika mikoa na wilaya mpya
No comments :
Post a Comment