Muwindaji aliyemuua simba CECIL nchini ZIMBABWE hatokabiliwa na mashtaka yoyote.
Waziri wa Mazingira nchini ZIMBABWE, OPPAH MUCHINGURI
Waziri wa Mazingira nchini ZIMBABWE, OPPAH MUCHINGURI amewaambia
waandishi habari kuwa, WALTER PALMER daktari wa meno na raia wa
MAREKANI, alikuwa na vibali vyote vinavyohitajika kuwinda simba nchini
humo.MUCHINGURI amesema serikali ya ZIMBABWE itatathmini zaidi namna vibali vya uwindaji vinavyotolewa.
CECIL alikua maarufu miongoni mwa watalii pamoja na watafiti ambapo
hapo awali PALMER alituhumiwa kumuua CECIL kwa kutumia upinde wa
kuwindia
No comments :
Post a Comment