Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuzindua awamu ya kwanza ya
mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani unaotarajia
kugharimu dola za Marekani bilioni kumi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
Dr. Florens Turuka, mradi huo unajumuisha eneo la hekta 800 kwa ajili
ya ujenzi wa bandari na eneo la hekta 1,700 kwa ajili ya ukanda wa
Viwanda.
Taarifa hiyo imesema mradi huo pia utahusisha ujenzi wa miundo mbinu
kama vile reli, mitandao ya barabara, umeme na mitandao ya mawasiliano
na utakapokamilika utaifanya Tanzania kuwa kituo kikuu cha usafirishaji
kwa wafanyabiashara wa ndani na nje
No comments :
Post a Comment