Obama amesema kuwa majeshi ya Afghanistan haviwezi kuhimili
vitisho vya Taliban
Rais wa Marekani,Barack Obama
ametangaza kuongeza muda wa majeshi ya Marekani kuwepo nchini Afghanistan.
Takriban wanajeshi 10,000
wataendelea kubaki nchini humo kwa kipindi hasa cha mwaka ujao.
Wakati ambapo Rais Obama anaondoka
madarakani mwaka 2017, kutakuwa bado kuna wanajeshi 5000 nchini Afghanistan.
Obama amesema vikosi vya Afghanistan
havina nguvu bado ya kupambana na tishio linaloongezeka kutoka kwa wanamgambo
wa Taliban.
Washington pia imesema inatarajia
kuendelea kuungwa mkono na washirika wake, na kuwa mazungumzo kuhusu suala hili
yamekwisha anza.
Obama ameweka wazi kwa Taliban kuwa
makubaliano ya kisiasa na Serikali ya Afghanistan kutafanya majeshi ya Marekani
yaondoke Afghanistan
No comments :
Post a Comment