Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta amepuzilia mbali onyo la jaji wa mahakama ya ICC Chile
Eboe-Osuji ya kuwataka wakenya wakome kuijadili kesi inayoendelea
kusikizwa dhidi ya Naibu Rais wa Kenya William Ruto na mwandishi wa
habari Joshua Sang.
Jaji Eboe alionya wanasiasa wanaoitukana
mahakama hiyo hususan katika mikutano ya hadhara ya maombi ambayo imetia
fora nchini Kenya.
Akilihutubia taifa katika hafla ya kuadhimisha sikukuu ya mashujaa, Rais Kenyatta amesema
''hata
wale wanaotusukumie hii mambo ya icc kila siku mambo ni ICC wawachane
na sisi wawache sisi tuendeleee kujenga na kuunganisha wakenya
wenzetu.''
''Na sisi wakenya tuendelee kuomba jaji fulani
hawezi kutuambia ati sisi hatuna nguvu ya kuomba ... sisi tunaamini
mungu, Na sisi tunauhuru wa kuomba, Na tutaendelea na maombi kwa sababu
tunajua maombi faida yake ni nini'."
Uhuru alisema akiashiria onyo la Jaji Chile Eboe-Osuji anayesikiza kesi dhidi ya Ruto na Sang.
Kenyatta alisema kuwa mikutano ya maombi ya kumuombea naibu wake itaendelea.
Naibu wake William Ruto na muandishi habari Joshua
arap Sang wanakabiliwa na tuhuma za kuchochea mapigano yaliyosabisha
vifo vya watu 1,300 huku wengine laki sita wakihamishwa makwao punde
baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007 kutangazwa nchini
Kenya.''
Jaji
No comments :
Post a Comment