Aliyekuwa
mwenyekiti mwenza wa chama cha UKAWA nchini Tanzania, Dkt. Emmanuel
Makaidi ambaye aliaga dunia siku tano zilizopita, alizikwa Jumanne mjini
Dar es Salaam.
Marehemu Makaidi alikuwa pia mwenyekiti wa chama cha
National League and Democrasy NLD, mojawapo ya vyama vilivyoungana
kuanzisha chama kikuu cha upinzani, UKAWA, kinachoongozwa na aliyekuwa
Waziri Mkuu Edward Lowasa.
Upinzani ulisitisha kampeni kwa muda wa saa 24 kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi huyo.
Viongozi wa tabaka mbali mabli walihudhuria mazishi hiyo katika makaburi ya Sinza mjini Dar es Salaam.
Makaidi alitarajiwa kugombea kiti cha ubunge katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili.
Kufikia sasa wagombea sita waliotarajiwa kuwania viti vya ubunge katika uchaguzi huo wameaga dunia
No comments :
Post a Comment