Urusi na Marekani zimetia saini makubaliano yanayotarajiwa kuzuia ndege za kijeshi za nchi hizo kushambuliana nchini Syria.
Habari za kutiwa saini kwa mkataba huo zimethibitishwa na maafisa kutoka nchi zote mbili.
Urusi
ilianza kushambulia kwa ndege maeneo ya Syria Septemba 30, ikisema
ilikuwa ikiwalenga wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS).
Wiki
iliyopita, Marekani ilisema ndege za mataifa hayo zilikuwa “zimeingia
eneo moja ya mapigano” na zilikuwa karibu sana kukutana.
Maafisa wa mataifa hayo wamekuwa wakitafuta mwafaka tangu mwishoni mwa mwezi Septemba.
Msemaji wa Pentagon Peter Cook amesema maelezo zaidi kuhusu makubaliano hayo yatasalia kuwa siri, kufuatia ombi la Urusi.
Hata hivyo, alisema mwafaka huo unaweka mikakati ya pande zote mbili kuwasiliana.
Nchi hizo mbili hata hivyo hazitaelezana habari za kijasusi kuhusu maeneo yanayolengwa na wanajeshi wa kila upande.
Bw
Cook alisema mkataba huo unahakikisha ndege za kila taifa zitakaa
“umbali salama” kutoka kwa ndege za taifa hilo jingine. Hata hivyo,
hakueleza umbali ulioafikiwa.
Wiki iliyopita, Pentagon ilisema
ndege za kijeshi za Urusi na Marekani wakati mmoja zilikuwa
zimekaribiana kiasi cha marubani kuweza kuonana, kilomita 15 hadi 30.
Waziri
msaidizi wa ulinzi wa Urusi Anatoly Antonov amesema makubaliano hayo
yameweka mikakati ya kuzuia kushambuliana kwa ndege za Marekani na
Urusi.
No comments :
Post a Comment