Vyama
vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA vimedai kubaini matatizo
kadhaa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ikiwemo baadhi ya kadi za
kupigia kura kuwa na picha za nyumba, pikipiki na maghala badala ya
watu.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam mkurugenzi
wa kampeni na uchaguzi Bw Regnand Munisi amesema tume kuchelewa
kutangaza idadi ya vituo vya kupigia kura kuwa viko wapi na vingapi
kunawafanya washindwe kuandaa mawaka la mapema.
Naye makamu mwenyekiti wa Chadema bara Prof Abdala Safari amesema
kutokana na masuala mbalimbali yanayojitokeza hivi sasa ikiwemo serikali
kuingilia kazi za tume ya uchaguzi na vitisho vinavyotolewa
wanaiandikia jumuia ya kimataifa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC
barua kuhusu suala la wananchi kupiga kura na kubaki mita mia mbili nje
ya eneo la kituo cha kupigia kura mwanasheria wa chama hicho amesema.
No comments :
Post a Comment